KAGOMA GREEN ESTATES
Thursday, 15 October 2015
Friday, 2 October 2015
Kilimo cha Umwagiliaji
Mfanyakazi wa Kagoma Green Estates akivuta mpira wa kumwagilia miche ya ndizi kwenye shamba la kampuni hiyo katika kijiji cha Kikuku Wilaya ya Muleba Kagera
Kagoma Green estates kuongeza thamani ya zao la ndizi Kagera
Mtanzania mzalendo ambaye ameamua kuonyesha juhudi zake za
kuondoa umasikini kuanzia kijijini alikozaliwa Ndugu Salum Said Seif kupitia
kampuni yake iitwayo Kagoma Green Estates ameamua kuwekeza katika zao la ndizi
ambalo anatarajia kuongeza thamani katika zao hilo kwa kuanzisha kiwanda cha
juisi ya asili inayotokana na zao hilo.
Akiwa mzaliwa wa kijiji cha Kagoma Salum mwenye kauli mbiu
ya “Mjini ni Pori” anaamini kwamba huko ndiko watu wanakoenda kukata kuni
wakimaliza wanarudi nyumbani kwa ajili ya kupikia, hivyo na yeye ameamua kurudi
kuwekeza nyumbani ili watu wengine waige ili watanzania wengi waondokane na
umasikini
Kagoma Green estates ambayo imeamua kuweka shamba kubwa la
mfano katika kijiji cha Kikuku Wilaya ya Muleba wamepanda ndizi za sukari kwa
ajii ya kutengeneza juisi ya ndizi na kampuni pia inajihusisha na uhifadhi wa
mazingira kwa kupanda miti katika sehemu mbalimbali na kulinda vyanzo vya maji
Akizungumza na waandishi wa habari Meneja mradi wa Kagoma
Green estates Bwana Sylivester Marosha Ihuya anasema mradi wao ni wa
kipekeenchini Tanzania kutokana kwamba utanufaisha wananchi wote wa Kanda ya
ziwa hasa wale wote wanaolima zao la ndizi.
“Mradi wetu umelenga kuondoa umasikini na pia mkurugenzi
wetu ambaye ni mzaliwa wa hapa anapenda kuona kile alichopata anagawana na
wananchi wake. Tunataka tuisaidie jamii ya hapa, tutanunua mazao yao na
kuwaletea maendeleo hapa walipo. Pia tumejitolea kujenga choo cha kisasa kwa
ajili ya Ofisi ya serikali ya kata Kagoma ” anasema Marosha
Marosha anasema kwamba ni mradi wa kusaidia zaidi jamii,
kuondoa umasikini na pia kuiendeleza Kagoma na kanda ya ziwa kwa ujumla hasa
kaya masikini ili wanufaike na mazao yao hasa zao la ndizi ambalo ndilo zao kuu
la chakula na biashara katika kanda ya ziwa.
“Tumeamua kulima ndizi ili tuiongezee thamani zao hili kibiashara kwa kuanzisha kiwanda cha kusindika juisi asili (organic juice) ambayo haitahitaji kuongezewa sukari kama matunda mengine” anasema Marosha
Anasema kwamba soko lao litakuwa kwanza Kanda ya ziwa na
badaaye juisi hiyo itasambazwa na maeneo mengine ya nchi ya Tanzania na
ikiwezekana na nchi za nje.
Tangu mradi wa Kagoma Green estates uanzishwe mapema mwaka
huu, jamii ya wananchi wa maeneo ya jirani wamenufaika sana kwa kujipatia ajira
ya kilimo, kuuza miche ya migomba, madereva wa kuendesha mitambo, wafanyakazi
wa umwagiliaji, walinzi na pia jamii imenufaika kutokana na shamba lao kuwa
shamba darasa.
“Wananchi wa hapa wamenufaika sana na wataendelea kunufaika
na kampuni yetu kutokana na shughuli zetu mbalimbali na pia shamba letu ni
shamba darasa.Wataalamu mbalimbali wa kilimo wanafika hapa kwa ajili kutoa
elimu inayohusu kilimo bora , matumizi bora ya ardhi na uhifadhi wa mazingira”
anasema Marosha
Kagoma Green estates pamoja na shughuli nyingine
imejidhatiti katika utunzaji wa mazingira kwa kuvilinda vyanzo vya maji. Ulimaji
wa shamba ni wakisasa kwa kutumia mbinu mbalimbali za kilimo cha kisasa
“Unaona hapa tuko maili nyingi karibu mita 200 kutoka katika
vyanzo vya maji na pia umwagliaji wetu katika shamba letu ni wa kisasa. Tunatumia mabomba kumwagilia na
umwagiliaji wa drip (drip irrigation). Wafanyakazi wetu wanatumia vifaa bora
vya kilimo na katika kupanda hatutumii mbolea za kemikali” anasema
Naye msimamizi wa shamba Bwana Projestus Francis (32)
anasema tangu azaliwe hajawahi kuona mradi kama huo unaletwa kijijini kwao huku
akisema umekomboa vijana wengi wa kijijini hapo ambao walikuwa hawana shughuli
maalumu.
“Sina cha kusema ni mradi wa kihistoria ambao mimi na
familia yangu hatutakuja kusahau. Mimi shughuli yangu hapa ni kuangalia kila
kitu kinacholetwa hapa nakipokea mimi na kutoa risiti” anasema Projestus
Anasema vijana wengi kijjini hapo na vijiji vya jirani
wamepata ajira ya maana kwa sababu kila siku mwenye bidii anaondaka na shilingi
20,000/= kama ujirra wa kibarua. Hii ni pesa nzuri sana ukilinganisha walio
wengi tulikuwa hatuipati hapo kabla
“Malengo yangu kama mungu atasaidia yatatimia kwa sababu
ninachopata hapa kinanisaidia sana mimi na familia yangu ambayo ina watoto
watatu.Ninachoweza kusema ni kwamba vijana wachangamkie fursa hii haraka waje
tuunde kikundi tufanye kazi kwa Kagoma Green estates kwa pamoja ili tunufaike
na mradi huu” anasema.
Pia kijana wa kisukuma ambaye amesafiri na wenzake kutoka
Mwanza ambaye amekuja kuichangamkia fursa katika shamba la Kagoma Green estates
Bwana Jonsina Makwaya anasema amefarijika sana kuona mradi huo unaletwa Kanda
ya Ziwa.
“Nimetoka Mwanza kuja kulima hapa na mazingira ni mazuri
muno hapa na mradi huu ni wa kipekee kwa sababu pesa tunayolipwa hapa inakidhi
mahitaji yetu hapa. Tumepewa nyumba tunaishi, tunakula na tunalipwa pesa nzuri
nawashauri vijana waje wachangamkie fursa hii” anasema.
Subscribe to:
Posts (Atom)